Saturday, September 25, 2010

VODACOM MISS TANZANIA YAFIKIA TAMATI….!!!

Toka habari zianze kurindima katika vyombo vya habari nchini yapata mwezi sasa na tumekuwa tukiwaona katika shughuli mbalimbali za kijamii hatimaye kiu ya wapenzi wa shindano hili ilikidhiwa usiku wa kuamkia tahere 12/9/2010 katika viwanja vya Mlimani City ndani ya wilaya ya Kinondoni.
Mshindi toka Wilaya ya Temeke Genevieve Emmanuel Bila ya kuamini masikio yake alitajwa kuwa mrithi na mmliki mpya wa taji la Miss Tanzania 2010.
01.jpg
Vodacom Miss Tanzania 2010 Genevieve Emmanuel   (katikati) akiwa na washindi wenzake mara baada ya kutangazwa mshindi kwenye shindano hilo lililofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam siku ya Jumamosi  (kulia) ni mshindi wa tatu Consolata Lukosi na (kushoto) ni mshindi wa pili Glory Mwanga

No comments: