Monday, September 20, 2010


Sophia Juma akiwa hoi baada ya kupokea simu asiyoitambua.
“Rajabu alidai alipigiwa simu namba 068400000 na kupatwa na mshituko na kupooza, lakini ripoti ya kitaalamu bado sijapewa, hivyo naomba mnipe muda ili wataalamu wafanye kazi yao kwanza, bado kalazwa kwa uchunguzi,” alisema Kamanda Kaluba.

Hata hivyo, kulikuwa na taarifa kuwa mtu mwingine mkazi wa Kata ya Tumbi, Kibaha ambaye jina lake halikuweza kutambulika mara moja alipatwa na tukio kama hilo na kulazwa katika Hospitali ya Tumbi, lakini sasa ameruhusiwa baada ya matibabu.

Tukio kama hilo pia liliwahi kutokea katika eneo la Mwanjelwa, Mbeya ambapo msichana mmoja alilazwa katika zahanati moja baada ya kupokea simu iliyotoa maandishi ya Call 1 na inadaiwa ilimsababishia mwili wake upande mmoja kupata ganzi na baada ya matibabu akaruhusiwa kurudi nyumbani.

Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili, waliitaka Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) kufanya uchunguzi wa kina na wasiishie kutoa majibu ya mkato kuwa hakuna tatizo kama hilo.

Habari zaidi zinadai kuwa tukio la kifo cha Mkurugenzi Msaidizi wa Bendi ya Diamond Music, Pafect Kagisa ‘P Diddy’ kilichotokea hivi karibuni jijini Dar es Salaam, kinachodaiwa kilitokana na kupokea simu, kimeingia katika sura mpya baada ya kudaiwa kuwa polisi watalichunguza.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Elias Kalinga alisema jana kuwa suala hilo ni la kitaalamu na kuwa hawezi kulitolea jibu mpaka hapo atakapolifanyia uchunguzi.

Pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA kuwatoa wasiwasi Watanzania juu ya uvumi ulionea nchini kuwa namba za simu zikipokelewa huleta madhara na hata kifo kwa mpokeaji, bado uvumi huo unaendelea na katika mahojiano haya, gazeti la Uwazi limeongea na Bi. Sophia Juma ambaye amedai kupatwa na matatizo ya kuishiwa nguvu na mkono kufa ganzi mara baada ya kupiga namba ya simu asiyoijua...msikilize mwenyewe!!

Wakati hayo yakitokea hapa nchini, jirani zetu wa Kenya wananchi wao kadhaa wamelalamika kukumbwa na matukio kama hayo.
Wananchi hao wamedai kuwa namba ambazo zimewaathiri baadhi ya raia wa huko ni 8888308001, 931604812191,9876266266211, 9888854137 na 9876715587. Waziri wa Habari na Mawasiliano wa Kenya, Samweli Poghisio alikiri kupokea madai hayo lakini akatoa wito kwa kuwataka wananchi waache kusambaza ujumbe wa aina hiyo na ameyataka makampuni ya huduma za simu kutayarisha orodha ya namba za simu zinazotumika kusambaza ujumbe huo ili polisi wafanyie kazi.

Hivi karibuni, Mkurugenzi wa Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkhoma amekanusha mara kadhaa kuhusu hali inayowatokea watu katika maeneo tofauti na kudai kuwa huo ni uvumi na hofu za watu wenyewe
Imeandikwa na peter duwe

No comments: